Aidha, Sheikh Dkt.Alhad Mussa Salum, ametumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa niaba ya JMAT na ambapo alisema: "Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT-TAIFA) inatoa pongezi za dhati kwa familia ya Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na kuwaombea wanandoa wapya maisha yenye upendo, baraka na amani ya kudumu".
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Dar es Salaam, [18-08-2025] - Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT-TAIFA), Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum, alipata wasaa wa kushiriki katika hafla ya harusi ya mtoto wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Masheikh maarufu, waumini pamoja na wageni kutoka kada mbalimbali za kijamii.
Katika hotuba yake ya pongezi, Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum alisisitiza kuwa:
“Harusi ni jambo la kheri, na watu wema na wenye kheri katika jamii daima hufanya lenye kheri na huonekana wakishiriki katika mambo ya kheri.”
Hafla hiyo ilifanyika katika mazingira ya furaha, mshikamano na upendo wa kijamii, ikidhihirisha Ushirikiano wa kidini na kijamii miongoni mwa wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Aidha, Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa niaba ya Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT-TAIFA) ambapo alisema:
“Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT-TAIFA) inatoa pongezi za dhati kwa familia ya Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na kuwaombea wanandoa wapya maisha yenye upendo, baraka na amani ya kudumu.”
Your Comment